MAMBO YA KI-STONE

Wengi wetu wanafaulu vizuri sana Darasani lakini wakiwa makazini ni watendaji wa ovyo oyo tu yaani hawana jipya.Binafsi hawa nimekutana nao wengi tu kiasi

nawasikitikitia sana.Maranyingi najiuliza je ni ubovo wa elimu yetu au ni vilaza tu? Rafiki yangu ana diploma ya I.C.T kasoma pale UCC anachojua yeye ni adobe photoshop tu.Hajui process za windows installation,na vingine vingi lakini kwa notes aisee yuko vizuri sana.

         Nachotaka kushare nanyi ni kuhusu elimu ya computer ya mtaani.Nikisema ufundi hata wale wapiga "windows"siku hizi wamekuwa na ofisi wanasema IT technicians yap wanafanya vizuri tu si vifaa vyenu vinapona pale wanapootea?Uzuri wa computer sofware haidanganyi eti uegeshee tu kwa kubambika NOOOOO! kama unajua unajua tu. Unaweza kuwa na Diploma ya Darasani  na masters ya Kitaani kama utazingatia yafuatayo.

1.Kuwa mdadisi na anayependa kujifunza kila siku Computer hubadilika kila uchwao kisoftware ingawa Hardware ni ileile lakini Tambua kuwa ili Hardware iende yahitaji software 

2.Usikubali kushindwa kirahisi pambana kwa fact na usilazimishe usichokijua kuwa na uhakika na step

unayochukua.Kumbuka kosa dogo tu litakugharimu

3.Hata kama mkali kiasi gani fuata hatua muafaka za kiufundi ama sivyo zitakughalimu,hapa kuwa mtu na mbunifu mwanzoni nilikuambia nenda na wakati.(be upto dated)

4.Fafanua kila tatizo kwa njia Rahisi,usilifanye kwa njia ngumu kuonyesha unajua ili upige pesa unaajipotezea muda kumbukaa husubiliwi.

5.Kuwa na utaratibu wa kuhakiki kazi yako mara baada ya kuimaliza.Fanya majaribio ya mara kwa mara weka kumbukumbu ya njia uliyoitumia kutatua tatizo lililokuumiza kichwa kisha share na washikaji ulipofanikiwa na ulipokwama



Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Java kidogo kwa wale wanaoanza

Chakachua moderm yako korofi ya ZTE itumie line zote daima kwa QPST