Mobile Phone:Apps,Tricks&Hardware
Geuza Smartphone Yako Kuwa Computer
Unajua Kama Ukiwa Na
Smartphone Unaweza Kuigeuza Ikawa Computer?
Leo Nimekuja na kitu
kizuri!
Ni moja ya mambo ya
Ukuaji wa teknolojia, hivyo basi sio mbaya baada ya kukushirikisha
ukamshirikisha na mwenzako pia;
- Ulishawahi kuhisi kuichoka simu au tablet yako kutokana na udogo wake kwenye kuhifadhi mambo yako? (low storage space)
- Muda mwingine inakusumbua na kukwambia memory is full huwezi kuweka kitu chochote
- Simu yako imejaa vitu vyako vya muhimu sana na hauna Computer na hautaki kuvifuta na pengine hauna sehemu ya kuvitunza
- Ukisoma maelezo vizuri utagundua vingi na utapata njia ya kutatua matatizo mengine mengi pengine hata yakazidi hayo niliyoyataja hapo
Ok, sasa basi ninakupa
hii kitu hapa, Kuna Cable Mpya kabisa zimetoka juzi juzi zinaitwa “OTG Cables“, kirefu cha OTG ni (On The Go) Kwa hiyo kwa kirefu
zinaitwa On The Go Cables, Hizi Cable kuna watu hawazifahamu kabisa na hawajui utamu wake.
Leo nakudadavulia mambo makubwa utakayoweza kuyafanya endapo una OTG Cable, itazame hapa;

Cable hizi zina pande
mbili,
Upande wa kwanza una
kichomekeo kama Cha zile chaji za smartphones zetu tulizozizoea, na huu ndio
upande unaoingia kwenye simu au tablet na unachomeka kama vile unavyochomeka
chaji.
Na upande wa pili wa OTG Cable kuna tundu kubwa la kuchomekea vitu vya asili za USB kama vile flash, lakini kwa upana zaidi naomba nieleze maana kuu ya hili
tundu (kwa kitaalamu huwa tunaliita USB Female Port), na linaruhusu
kuchomekwa vifaa mbalimbali kwa matumizi tofauti tofauti ila tu vifaa hivyo
viwe vya aina ya USB, mfano kama Flashi, Keyboard, External
Hard Disk, Speakers n.k.
Sasa basi ukichomeka
Cable hiyo kwenye simu au tablet yako kama vile unavyochomeka chaji kwa upande
wa kwanza na upande ule wa pili ukachomeka flash, basi utaweza kuisoma kwa
ndani ya simu kama vile huwa unasoma memory card yako, tazama picha hapa chini
kuelewa zaidi;
Unaweza pia kuchomeka External Hard Disk na
ukaitumia kwenye simu au tablet yako, kufanya shughuli mbalimbali kama vile
kucheki movies n.k, sijamaliza bado;
Kama simu au tablet yako
imejaa vitu unaweza kuvihamishia kwenye flash ukavitunza, kwa mfano hauna
Computer, unaweza kununua OTG
Cable na flash yako ya 16 GB ukaweka vitu vyako kama Picha,
Videos n.k na simu yako ikabaki free na ikawa na spidi ile ile kama ya siku
ile ulipoinunua, na hapa hautalalamika tena kuwa simu yako ina uwezo mdogo wa
kutunza vitu, sijamaliza bado;
Kwa wale tunaotamani
sana kuwa na Computer lakini hatuna uwezo wa kuzinunua, lakini
tunamiliki Smart Phones Zetu nzuri tu, basi hapa nakupa maujanja, nenda dukani
ulizia OTG Cable (Sijui ni duka gani maana simtangazii mtu biashara ila mimi
binafsi nilinunua elfu 5 tu ila kuna sehemu ukienda utapigwa mpaka elfu 40,
tembelea duka lolote la simu ulizia), ukishanunua OTG Cable, nunua flash zako za 16 GB kama 3 au 5 kama una uwezo, kisha
nenda kakopi vitu unavyohitaji kwa mtu mwenye Computer na uviweke kwenye flash
yako (mfano flash ya Movies pekeyake, ya madocuments pekeyake, ya miziki
pekeyake na ya picha pekeyake, najua ugonjwa wetu vijana na wazee kwa mbaliii
ni Miziki, Movies, Kujirekodi Na kupiga Picha hasa kwenye event za kifamilia na
hivi vitu hujaza sana simu zetu, hivyo ukiwa na flash zako kama nivyoeleza basi
utakuwa salama zaidi, ukiweza hayo basi Ukiwa na simu yako, flash zako,
na hiyo OTG Cable ni sawa na kumiliki Laptop, sijamaliza bado;
Utaepuka maswala ya
kuhamisha vitu kwa kuchomeka USB cable, au kutumia bluetooth kuhamishiana vitu
vyenye saizi kubwa na vingi toka kwenye simu au tablet ya mtu mwingine
bali litakuwa ni swala zima la kuchomeka OTG Cable na flash yako kisha
unahamisha vitu kwa kukopy na kupaste, na zina spidi nzuri balaa, sijamaliza bado;
Wale wenye simu kubwa
unaweza kuikamilisha simu yako kuwa Computer kwa kuifanya hiyo OTG Cable iweze kuzalisha USB ports nyingine nyingi ili uweze kuchomeka
vifaa vingi kwa wakati mmoja kama Speaker, keyboard, mouse,
external hdd n.k, angalia picha hapa chini;

Jamani kuna mengi
yanakuja mazuri tu usisahau kuwa unatembelea na site hii kwani kuna mengine
yatakupita, kwa wale wa mikoani mnaohitaji kujifunza Ufundi wa Computer kwa
njia ya Mtandao soma kila kitu kisha nitafute tuyajenge, nakutakia Jumapili njema
Comments
Post a Comment
solate forever