Computer:Software,Tricks & Hardware
Zuia Kuibiwa Vifaa Vya Ndani Vya Computer Yako
Kwanza kabisa unatakiwa
ufahamu kuwa sio rahisi kuweza kufahamu kila kifaa cha Computer yako kilicho
ndani, lakini hapa ninakuwezesha kufanya hivyo kwa njia nyepesi kabisa.
Leo nimekuletea Software
maalum kabisa kwa ajili ya kulist/Kuorodhesha kila kilichomo ndani ya Computer
yako, kwa majina pamoja na Model zake, hivyo basi unaweza kuvirekodi pembeni
hata ktk Diary yako kwa usalama zaidi, ili ikitokea umetofautiana na fundi wako
basi unafungua software yako na kisha unaiomba ikuorodheshee vifaa vya Computer
yako na hapo utaweza kucompare kama ni vilevile ulivyovirekodi mwanzo au sivyo,
na mwisho kabisa utafahamu ukweli uko wapi.
Uzuri wa software hii
ni kwamba;
- Haina saizi kubwa (MB 4.9 tu)
- Ni rahisi kutumia
- Haina kona nyingi wakati wa kuinstall
Zifuatazo ni hatua za
kuinstall kisha majibu yote leta Facebook;
- Utadownload software hii kwa kupitia link nitakayoitoa hapa chini
- Utainstall kama kawaida
- Wakati wa kuinstall haitaomba password na ni free kabisa
- Ukimaliza kuinstall nenda kwenye desktop kisha itafute utaona imeandikwa “Speccy”
- Double click/Ibonyeze mara 2 harakaharaka ili kuifungua
- Ikifunguka itakuja kama hivi inavyo onekana hapa chini

Sasa basi hapo unaweza
kuona mwenyewe vitu gani vimeorodheshwa kwa majina, saizi pamoja na modeli
zake, kwa mfano;
- CPU/PROCESSOR/(UBONGO WA COMPUTER)
- RAM/(VITUNZIO VYA DATA KWA MUDA ZINAOTUMIKA)
- MOTHERBOARD/(KIFAA KINACHOUNGANISHA VITU VYOTE NDANI YA COMPUTER)
- STORAGE/HARD DISK/(KIFAA KINACHOTUNZA DATA ZAKO ZOTE)
- N.K
Wengi wetu huibiwa RAM, HDD, MOTHERBOARD
na PROCESSOR, hivyo basi unatakiwa kufahamu vitu vidogo kama hivi ili
kuepusha matatizo na mtu, na sio lazima awe fundi tu, wapo hata marafiki wasio
waaminifu ambao tunawaazima Computer lakini zinarudi zimebadilishwa vitu.
Sasa basi download Hii
software kwa kubonyeza link hii;
Comments
Post a Comment
solate forever