Swali toka kwa
                       Dr.Lugakingira wa Bunju:
             Natumia Dell Latitude 610,Nime"install" camera (webcam) kwenye mashine yangu Process za kuinstall zinaenda vizuri lakini wakati wa kuitumia ina andika your computer has no video hardware Naomba msaada hapo nimekwama nahitaji kutumia webcam ya nje natumia windows 7
 
Jibu la Technician:
               Nashukuru kwa swali lako dokta,kiasili dell latitude haina web cam ndio maana unatumia extenal webcam.Hardware inayouliziwa hapo ni hiyo camera{webcam}.Zingatia yafuatayo ili uweze kuitumia
(1)Mara nyingi Vifaa kama hivyo huja na cd(software yake).Hakikisha una hiyo cd,na kilichopo humo 
     ni software ya hiyo camera halisi kama huna sofware inayoendana na kifaa chako ukiweka nyingine 
      lazima utapata ujumbe kama huo maana hakuna muunganiko kati ya software na Hardware Hapo wewe
     unatumia software bila hardiware kutambulika
(2)Nenda kwenye device manager angalia kama computer yako imeitambua hiyo camera yako kama imeshindwa kuioanisha utaona kuna alama ya mshangao kwenye hiyo device.hapo weka software yenye kufanana na camera.
(3)Zima computer na washa tena angalia kama tatizo limetatuka
(4)jaribu kutafuta online sofware mpya ya hiyo webcam yako au tutembelee ofisini kwetu kwa msaada zaidi

Comments

Popular posts from this blog

Jifunze Java kidogo kwa wale wanaoanza

Chakachua moderm yako korofi ya ZTE itumie line zote daima kwa QPST